Ijumaa , 8th Jul , 2016

Wafanyabiashara wawekezaji kutoka nje ya Tanzania wametakiwa kuacha tabia ya ukwepaji kulipa kodi kwa wakati kwani kwa kufanya hivyo kunalisababishia taifa hasara ya kodi ambayo kama ingekusanywa kwa wakati ingebadilisha maisha ya wananchi.

Wafanyabiashara wawekezaji kutoka nje ya Tanzania wametakiwa kuacha tabia ya ukwepaji kulipa kodi kwa wakati kwani kwa kufanya hivyo kunalisababishia taifa hasara ya kodi ambayo kama ingekusanywa kwa wakati ingebadilisha maisha ya watanzania walio wengi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwakilishi wa wauzaji wa Mafuta nchi Bw. Victor Ndamgoba amesema kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kutokuwa waaminifu katika biashara zao, ni wakati sasa serikali ibadilishe adhabu kwa wakwepaji wa kulipa kodi nchini.

Bw. Ndamgoba pia amewataka wamiliki wa makampuni mbalimbali nchini wazingatie sera ya kutoa ajira kwanza kwa wazawa sambamba na kuangalia vigezo vya kazi zinazotolewa .