Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC, Beng'i Issa
Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC, Beng'i Issa wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa wawekezaji wa gesi na Petroli toka nchi mbalimbali.
Bi. Beng'i amesema mazingira bora yanaendelea kuwekwa na serikali yataiwezesha nchi kufaidika na kukochochea maendeleo kwa haraka na kuongeza kuwa amani na Utulivu uliopo unachangia kuiweka nchi mahali pazuri.
Mkutano huo uliwakutanisha wawekezaji wa kampuni kubwa za kimataifa duniani za gesi asilia na mafuta kutoka Marekani,Uingereza, Afrika Kusini,Norway, na Ujerumani pamoja na nchi za Afrika Mashariki.