Watumishi Geita wakamatwa kwa rushwa ya laki moja

Jumapili , 18th Apr , 2021

Taasisi ya Kuzuia na Kupamabana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita, imewakamata watendaji wa vijiji 30 kutoka wilayani Nyang’hwale kwa tuhuma za kugawana milioni 32 walizokusanya kupitia mashine za mfumo wa manunuzi ya umma kisha kuziharibu. 

Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Geita Leonidas Felix (katikati).

Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Geita Leonidas Felix amesema mbali na watendaji hao 30 wa Vijiji pia imewakamata watumishi wawili, Mkea Wambura (Afisa afya) na Emmanuel Madirisha mwanafunzi kutoka chuo cha Muhimbili baada ya kupokea malalamiko kuwa wameomba rushwa kutoka kwa mmiliki wa kiwanda 

''Tulipokea malalamiko kutoka kwa mmiliki wa Kiwanda kidogo cha kubangua Korosho ili wasimkamate baada ya kumkuta na mapungufu hivyo wakaomba rushwa kiasi cha shilingi  laki moja,'' amesema Kamanda Leonidas Felix.
 

Tazama Video hapo chini