
Bomu hilo lililipuka wakati watu walipokuwa wakifurahia usiku mmoja wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Hili ni shambulio baya zaidi kuwahi kutokea nchini Iraq tangu uvamizi wa Marekani mwaka 2003.
Kundi la Islamic State (IS) limekiri kutekeleza shambulio hilo. IS imeshindwa na kupoteza udhibiti wa maeneo, lakini bado inaendelea kufanya kazi.
Mauaji hayo yalifanyika Jumapili au Jumatatu, ofisi ya waziri mkuu Mohammed Shia al-Sudan imesema. Hakutaja majina ya waliouawa.
Waziri mkuu alizifahamisha familia za wahanga kwamba "adhabu ya haki ya hukumu ya kifo" imetekelezwa dhidi ya "wahalifu watatu muhimu waliopatikana na hatia ya kuhusika na shambulio la kigaidi", ofisi yake imesema.
Mnamo Julai 3, 2016 gari lililokuwa limejaa vilipuzi lililipuliwa karibu na kituo cha ununuzi kilichojaa watu katika mji wa Karrada, eneo ambalo ni la Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mji mkuu wa Iraq.
Wengi wa wahanga waliuawa na moto ulioteketeza jengo hilo baada ya mlipuko wa bomu