Moja ya gari zilizopata ajali
Gari aina ya Toyota Land Cruiser lililokuwa limebeba waandishi wa habari waliokuwa wanakwenda wilayani Ukerewe kwenye ziara ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo, limegongana uso kwa uso na gari ndogo ya abiria (Hiace) na kusababisha vifo hivyo.
Picha ya gari lililopata ajali
Taarifa kutoka Ofisi ya Mkoa wa Mwanza zinaeleza kuwa ziara hiyo imeahirishwa huku wakibainisha kuwa miongoni mwa watu watano waliofariki pia yupo Ofisa habari na mahusiano wa mkoa wa Mwanza Bwana Abel Ngapema.
Watu wakitoa huduma ya kuwatoa majeruhi eneo la ajali
Wengine waliofariki ni wanahabari Husna Mlanzi wa ITV, Vanny Charles wa Icon, Johari Shani wa Uhuru Digital.
Miili ya waliofariki imehifadhiwa katika Kituo cha Afya Nassa wilayani Busega mkoani Simiyu.