Jumatano , 29th Jun , 2016

Mashambulizi ya kutumia bunduki na bomu katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Ataturk Jijini Istanbul yameuwa watu 36 na kujeruhi wengine zaidi ya 140.

Maafisa wa Uturuki wamesema washambuliaji watatu walifyatua risasi katika eneo la kuingilia uwanja huo jana na kisha kujilipua baada ya polisi kuanza kuwarushia risasi.

Waziri Mkuu Binali Yildirim amesema kuna viashiria vya awali vinavyoonyesha kuwa kundi linalojiita Dola ya Kiislam (IS) linahusika na shambulio hilo.