Jumanne , 19th Jul , 2022

Katibu Tawala wilaya ya Mtwara Thomas Salala, amesema kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakikwepa majukumu ya kulea watoto wao na badala yake watoto wengi kulelewa na  bibi na babu, hali ambayo husababisha watoto kukosa upendo na kuleta madhara kwa Taifa na jamii kwa ujumla.

Katibu Tawala wilaya ya Mtwara Thomas Salala

Hayo ameyasema mkoani Mtwara na kuongeza kuwa watoto wengi mkoani humo wanakosa malezi na makuzi toka kwa wazazi wao, hali inayodaiwa wengi wao kukosa uzalendo kwa nchi yao.

Baadhi ya wakazi wa mkoa huo wamekiri kuwapo kwa tatizo hilo huku sababu kubwa ikielezwa kwamba vijana wengi mkoani humo, hawapendi kushiriki  katika shughuli za maendeleao hali inayaopelekea baadhi yao kushindwa kutimiza jukumu la kuwalea watoto wao.