Watoto wanaozaliwa na jinsi mbili wasifichwe

Jumatano , 7th Jul , 2021

Jamii imeombwa kutowaficha watoto wanaozaliwa na jinsi mbili tofauti badala yake kuwafikisha kwenye mamlaka husika za serikali ili waweze kupimwa na kufanyiwa uchunguzi wa kitaalum zaidi.

Mkurugenzi wa Huduma na Udhibiti anayesimamia Uingizaji, Usambazaji na Matumizi ya Kemikali nchini kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Daniel Ndiyo .

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma na Udhibiti anayesimamia Uingizaji, Usambazaji na Matumizi ya Kemikali nchini kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Daniel Ndiyo ambaye amesema watoto wanaozaliwa na jinsi mbili wapo ijapokuwa jamii inawaficha.

"Kwa sasa hakuna haja ya kuwaficha watoto hao, GCLA inatoa huduma ambapo kwa kushirikiana na madaktari mbalimbali wanafanya uchunguzi wa kuthibitisha ni jinsia  gani ambayo inatawala kati ya kiume na ya kike," amesema Daniel.

Amesema wanapofanya uchunguzi wa kimaabara wanaweza kutambua kwamba mtoto huyo ni mwanamke au ni mwanaume hivyo jinsia ambayo inatawala ambayo haitakiwi kuwepo wanawashauri madaktari kuweza kufanya upasuaji ili kumuwezesha mtoto huyo atambulike kama ni mwanaume au mwanamke.

Aidha, Daniel amesema kuwa mamlaka hiyo inafanya uchunguzi wa vinasaba kwa wagonjwa wa figo wakati wa kuhitaji mtu wa kumuwekea figo hiyo.