Alhamisi , 22nd Sep , 2022

Watoto wawili wa familia moja waliogongwa na basi la Machame Investment Septemba 21 majira ya saa 12.30 asubuhi wakati wakienda shule mkoani Kilimanjaro wamezikwa leo huku Polisi wakitoa tahadhari

Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limesema halitasita kufunga leseni kwa baadhi ya madereva watakaothibitika kutotii sheria za usalama barabarani na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali vikiwamo vyombo vya moto.

Aidha Polisi imeomba ofisi ya katibu tawala wa wilaya ya Moshi kwa kushirikiana na halmashauri ya manispaa ya Moshi, kupanga vyema vituo vya waendesha pikipiki za kubeba abiria maarufu kama bodaboda, Bajaji na daladala katika maeneo ambayo havitaleta usumbufu kwa abiria wakiwamo wanafunzi.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema hayo wakati wa salamu za rambirambi za jeshi hilo kwenye mazishi ya watoto wawili wa familia moja waliogongwa na basi la Machame Investment Septemba 21 majira ya saa 12.30 asubuhi wakati wakienda shule.

Katika ajali hiyo basi la Machame lenye namba za usajili T 525 DZP liliendeshwa na Kombo Hassan  liliwagonga na kuwaua papo hapo watu watatu, waliotajwa kuwa ni Calistes Agust (57) aliyekuwa ambaye alikuwa bibi pamoja na wajukuu zake wawili Jesca Erick (9) mwanafunzi darasa la nne shule ya msingi Mawenzi Na Witness Audax (7) mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Muungano katika manispaa ya Moshi.

Akizungumzia ajali hiyo kamanda Maigwa amesema polisi inamshikilia dereva wa basi hilo….. na kwamba atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapomalika.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa chekereni ta bonite bw. ayubu juma aliomba jeshi la polisi kutoa mafunzo mbalimbali ya usalama barabarani kwa madereva pamoja na wanafunzi wawapo barabarani.

Nao baadhi ya washiriki latina misma hubo uliowaliza wazazi patoja na wote walioshiriki wamesema tukio hilo hawana budi kulipokea ila cha kikubwa ni sherry ifuatwe katika kupata haki za wahusika.