
Taarifa ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto iliyotolewa mwaka jana ilikiri kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi katika miji mikubwa ikiwemo jiji la Dar-es-Salaam, Arusha, Dodoma, Tanga, mwanza na Mbeya.
Katika kukabiliana na hali hiyo Wilayani Mbeya, Afisa ustawi wa jamii wa Wilaya hiyo THOBIAS MWALWEGO ameitaka jamii kutofumbia macho vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Kwa upande wake afisa habari wa halmashauri ya wilaya hiyo Hamza Mwangomale amesema maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afika kwenye halmashauri hiyo yatafanyika katika kata ya Mjele huku yakiwa na kauli mbiu ya ‘UBAKAJI NA ULAWITI KWA WATOTO WADOGO UNAWEZA KUEPUKIKA’.