Jumamosi , 3rd Dec , 2016

Kuelekea siku ya kimataifa ya kujitolea tarehe 5 Disemba, shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea UNV nchini Tanzania, linatarajia kuitumia siku hii kufanya kazi za kujitolea ili kuhamasisha jamii kujitolea kwa ajili ya maendeleo, amani na usaidizi

Mkuu wa wilaya ya Ilala akiwaongoza baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo katika kujitolea kufanya usafi.

Akizungumzia zoezi hilo afisa Programu wa UNV Joseph Aloo, amesema wamepanga kufanya usafi katika soko la Buguruni jijini Dar es salaam, ambapo pia watasheherekea kwa pamoja kwa wale watakao kuwa wamejitokeza kujitolea.

Ametaja faida za kujitolea kuwa ni pamoja na utoshelevu wa usaidizi kwa jamii na pamoja na kuwasadia vijana wengi kupata uzoefu wa kazi za kijamii ambayo itawasaidia kupata kazi zingine katika siku zijazo.