Alhamisi , 25th Feb , 2016

Watanzania wametakiwa kushirikiana na watunza kumbukumbu wa nyaraka na takwimu nchini kwa kujenga tabia ya kujisomea vitabu kwa lengo la kujiongezea upeo utakaosaidia kuinua uchumi wa taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni mstaafu Chiku Galawa akihutubia wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma ,Luteni Mstaafu Chiku Galawa alipokuwa katika mkutano mkuu wa umoja wa wakutubi nchini Tanzania ambapo amewataka watunza kumbukumbuku hao kuhakikisha wanatoa taarifa muhimu nchini.

Bi. Chiku amesema kuwa watumishi hao wasing'ang'anie kupata mshahara mkubwa wakati hawajawahudumia wananchi na kuendelea kutaka kutoa visingizio vya kutowahudumia wananchi ikiwemo kuwapa taarifa muhimu kupitia maandishi.

Mapema akiongea katika mkutano huo mwenyekiti wa chama cha wakutubi nchini Tanzania Richard Muhaha amesema kwa taarifa ambazo zinatolewa zinalenga kukuza na kutangaza rasilimali zilizopo nchini kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.