Jumatano , 6th Jul , 2016

Mbunge wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Mhe. Godluck Mlinga amewataka wanasiasa nchini kuacha tabia zakulipiza visasi kwa kuwanyima wananchi haki zao za msingi kwa kuwa uchaguzi umeisha na kazi iliyopo sasa nikuwaletea watanzania maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Mhe. Godluck Mlinga amewataka wanasiasa nchini kuacha tabia zakulipiza visasi kwa kuwanyima wananchi haki zao za msingi kwa kuwa uchaguzi umeisha na kazi iliyobakia sasa nikuwahakikishia viongozi hao wanawatumikia watanzania bila ubaguzi wa kiitikadi.

Mhe. Mlinga ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na East Africa Radio na kuongeza kuwa migogoro ambayo ilitokea wakati wa uchaguzi inapaswa kuachwa kwa kuwa watanzania wengi wanahitaji kutatuliwa matatizo yao ya sekta ya afya, elimu na yale ya kiuchumi kwa kuwapatia mitaji mbalimbali ambayo itaweza kuwasaidia kujikimu kimaisha.

Amesema kwa Jimbo la Ulanga vijana wenye sifa za kuendelea na masomo tayari amewaombea nafasi za vyuo takribani vijana 300 na wasionasifa zakuendelea na masomo ofisi ya mbunge itahakikisha inawapa mitaji mbalimbali ya ujasiriamali, kwa kuwa shughuli hizo zinazofanywa na vijana zinawasaidia sana vijana kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na la taifa kwa ujumla.

Mlinga amewashauri viongozi mbalimbali hasa wale wa vyama vya siasa nchini kuhakikisha wanajihusisha na shughuli mbalimbali ambazo zitawasaidia Watanzania kujikimu kimaisha na kuacha migogoro ambayo kama haitashughulikiwa mapema inaweza kuleta maafa makubwa ndani ya nchi.