Alhamisi , 8th Mei , 2014

Watanzania wametakiwa kujijengea tabia ya kuwa na bima za afya ili ziwawezeshe kupata huduma za matibabu kwa njia rahisi hata pale wanapokuwa hawana fedha taslimu mkononi na kuweza kuokoa afya zao.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, Jerry Slaa.

Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala Jerry Slaa wakati alipotembelea Hosipitali ya Aga Khan Kujionea namna inavyotoa huduma kwa wagonjwa wa Saratani ikiwa ni Taasisi ya Kwanza binafsi nchini Kutoa huduma hiyo ya matibabu ya saratani.

Aidha Meya Slaa amezishauri taasisi za binafsi za afya kutanua wigo wa huduma kwa kupeleka vijijini sambamba pia na kutoa wito kwa Watanzania kujijengea desturi ya kupima afya zao mara kwa mara ili kuzitambua afya zao mapema na kupata matibabu.