Makamu wa Rais Dkt Bilal katika mkesha wa mwaka mpya, uwanja wa taifa DSM
Onyo hilo limetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal alipokuwa mgeni rasmi katika ibada ya kitaifa ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2015 na kuliombea taifa amani,ibaada iliyofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, na kuwataka watanzania kuendelea kudumisha amani ya nchi
Dkt Bilal amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika matukio makuu ya kitaifa yanayotarajiwa kufanyika katika mwaka 2015, kubwa likiwa ni kura ya maoni kwa ajili ya Katiba mpya itakayofanyika April 30, pamoja Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba.
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka wananchi kudumisha amani na kuondokana na dhana ya ukabila ambayo itaondoa mshikamano uliopo miongoni mwa watanzania.
Aidha kamanda wa mkoa wa Kipolisi Temeke Kihenya Kihenya amesema kuwa mwaka huu wamejipanga kudhibiti matukio ya uvunjaji wa sheria na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi
Kwa upande wao wananchi wameelezea hisia zao katika kuupokea mwaka mpya na kuwataka viongozi waliowachagua kutimiza ahadi zao pamoja na serikali kutekeleza wajibu wake.