Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam na waziri wa nishati na madini mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo ambaye amesema kwa hali iliyopo kwa sasa kumekuwepo na ushindani mkubwa kwa wawekezaji hasa wawekezaji wa miradi mikubwa kama ya bomba la mafuta na gesi asilia hivyo ili wawekezaji wazawa wapate nafasi hizo ni muhimu wakatumia utaalamu walionao, umakini na uwezo kuliko kususubiri kubebwa kutokana na uzawa wao.
Profesa Muhongo ameongeza kuwa nje ya vigezo hivyo wazawa wataishia kulalamika kutokana na miradi hiyo mikubwa kuchukuliwa na watu wenye sifa na kuainisha kuwa ni vema kwa wazawa wakaimarisha taaluma na ujuzi ili waweze kupata watu wenye sifa ambao wataweza kushindana na mataifa mengine ya ndani ya bara la Afrika na nje ya bara la Afrika.






