Jumanne , 28th Jun , 2016

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba, amesema atawafukuza kazi warajisi wa vyama vya ushirika nchini kutokana kushindwa kusimamia vyama hivyo na kusababisha kufilisika na kutowadia wakulima.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba.

Waziri Tizeba ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa Wenyeviti, Makatibu na Mameneja wa vyama vya ushirika mjini Dodoma amesema mrajisi na warajisi wasaidizi anaowaongoza wana nafasi kubwa ya kuviangusha vyama vya ushirika.

Dkt. Tizeba amesema endapo mrajisi akifuta vyama zaidi ya 1800 nchini vilivyoshindikana basi pia ijiandae kuwafuta warajisi wote waliokuwa katika maeneo ambayo vyama hivyo vipo kwa kushindwa kuvisimamia vyama hivyo kutoa tija na wananchi.

Aidha, waziri huyo ametumia fursa hiyo kuwataka wenyeviti waliongilia masuala ya kifedha katika vyama vya ushirika wajitoe haraka na warudie majukumu yao ya kuviongoza vyama hivyo kwa mujibu wa sheria zilizopo kuhusu vyama vya vya ushirika.

Kwa upande wake Mrajisi na Mtendaji Mkuu wa Vyama vya Ushirika Dkt. Audax Rutabanzibwa, amevitaka vyama vya ushirika kufanya kazi zao zilizokusudiwa na si vinginevyo.

Sauti ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba