Ijumaa , 19th Jul , 2019

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Mwanza, imewapa tahadhari wananchi kuwa, ni marufuku kula nyama na pilau zitakazoandaliwa na wagombea watakaoshinda uchaguzi.

Pilau

Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoani humo, Leonida Felix, amesema wananchi wanapaswa kutambua kiongozi waliyemchagua, analo deni kwao la kuwaletea maendeleo kwa mujibu wa ilani ya chama chake, na si kwa wao kusherehekea ushindi huo kwa kupika na kula pilau.

''Pindi watakapokutwa na TAKUKURU wakipongezana kwa kula pilau na nyama zilizoandaliwa na mgombea aliyeshinda, watachukuliwa hatua za kijinai'',

Felix aliongeza kuwa, ''Sufuria za pilau na pilau yenyewe vitakuwa vielelezo mahakamani, vinavyoonesha uwepo wa mazingira ya rushwa'' amesema Felix.