
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu (Kulia)
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizindua kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia nchini.
Amesema katika kukomesha vitendo hivyo vya kikatili serikali imeandaa mpango kazi wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa mwaka 2017-2022 na kuanzishwa kwa madawati ya jinsia na watoto katika vituo vya polisi nchi nzima.
Waziri wa Afya - Ummy Mwalimu
Amesema marekebisho ya sheria ya elimu kwenye sura 353 kifungu cha 60 (1) kinachohusu adhabu kwa mtu anayempa ujauzito mwanafunzi tayari kimepitishwa na Bunge la 11 mwaka huu na kimeongeza adhabu kutoka kifungo cha miaka 3 hadi kufikia miaka 30, na kutoka faini ya shilingi 500,000 hadi 5,000,000.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika, Dkt. Judith Odunga amesema ni wajibu wa serikali kuboresha miundombinu rafiki kwa watoto wa shule ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa vyoo bora.
Kauli mbui ya mwaka huu ni 'Funguka pinga ukatili wa kijinsia elimu salama'.