
Jaji Joseph Sinde Warioba
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema kitendo cha kubaki na serikali mbili huku katiba moja ikisema hii ni nchi moja na Katiba nyingine inasema hizi ni nchi mbili kunaweza kuleta mgogoro utakaosababisha kuutikisa muungano.
Akihutubia mkutano ulioandaliwa na kituo cha Demokrasia Tanzania TCD wa tafakuri na maridhiano kuelekea katiba mpya jana jaji Warioba pia alisema maaraka ya bunge maalumu yanakuwa na mipaka endapo Rasimu ya katiba imeandaliwa na tume ya mabailiko ya katiba au chambo cha aina hiyo.Bunge la katiba linawewza kuwa huru kurekebisha baadhi ya masharti yaliyomo kwenye rasimu ya katiba lakini si suala la kawaida Bunge Maalumu kubadili hoja ya msingi.Jinsi ushirikishaji wa wanainch unvyokuwa wa wazi na mpana ndivyo madaraka ya bunge malumu yanavyopungua.
''Mantiki ni kuzuia Bunge Maalumu kunya'nya madaraka ya wanainch yaani"act of popular Sovereignty" wataalamu wa masuala ya katiba waaeleza kuwa madaraka ya Bunge maalumu katika mazingira haya ni kuboresha Rasimu ya katiba alisema Jaji Warioba.
Bunge maalumu la katiba litaanza kukutana jumainne ijayo kujadili Rasimu ya katiba iliyotolewa na tume ya mabadiliko ya katiba Desemba 30 mwaka ja.Jaji Warioba amesema bunge Maalumu la katiba linapaswa lifanye kazi ya kuboresha masharti ya kikatiba yaliyomondani ya Rasimu ya katiba pasipo kuweka masharti mapya abayo kwa kwa taadhira yake yanabadilisha au kufifisha yaliyomo kwenye Rasimu hiyo.