Kufuatia Mauaji hayo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agreya Mwanri, amezitaka Kamati za Ulinzi na usalama ngazi ya Mkoa na ile ya Wilaya ya Nzega kusitisha shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na sungusungu katika kijiji hicho.
Mwanri amesema kuwa amechukua hatua hiyo baada ya sungusungu hao kutekeleza mauaji hayo ya watu watano ambao wote ni wanawake wakituhumiwa kuwa ni washirikina.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa katika kuendelea kuchunguza tukio hilo jeshi hilo linawashikilia baadhi ya viongozi wa kijiji hicho ili kuweza kubaini waliotekeleza tukio hilo.
Msikilize hapa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agreya Mwanri pamoja na kamanda wa Polisi Wilbroad Mutafungwa wakitolea ufafanuzi juu ya tukio hilo.