Baadhi ya wanawake wa mkoa wa Simiyu, walioeleza changamoto waliyokuwa wakiipata sababu ya maji
Wakizungumza na East Africa Television, mara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji wa Nyakabindi Bariadi, mradi wa Nguno na Itilima Mjini uliofanywa na kiongozi wa mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Luteni Josephine Mwambashi, wananchi hao wamesema kero ya maji ilijeruhi ndoa zao, ingawaje kwa sasa wanakicheko.
Wamesema walikuwa wakipanga foleni kwenye visima vya maji kuanzia saa 9:00 usiku hadi saa 2:00 asubuhi, hivyo wameishukuru serikali kwa mpango wake wa kufikisha huduma hiyo ya maji safi na salama maeneo ya pembezoni.


