Jumatano , 6th Jan , 2016

Kwa miongo mingi nchi zilizoendelea zimekuwa zikimulika nchi zinazoendelea kama moja ya sehemu ambapo matukio ya uhalifu wa kijinsia,uvunjifu wa haki za binadamu pamoja na kutotii sheria kufanyika mara kwa mara.

Katika hali ya kushangaza Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, ameshtushwa na madai kwamba wanawake wapatao tisini walinyanyaswa kingono wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2016 mjini Cologne.

Polisi pamoja na mashuhuda wa matukio hayo wameelezea mashambulio hayo ya kingono kuwa yalitekelezwa karibu na eneo maarufu la cathedral, ambalo lilikuwa limefurika idadi kubwa ya makundi ya wanaume wenye asili na muonekano wa kiarab ama Afrika Kaskazini.

Merkel ametoa agizo la kufanyika uchunguzi wa kugundua ukweli kuhusiana na madai hayo na kisha kuwaadhibu wahusika, bila kujali asili yao ama historia za awali.

Meya wa mji wa Cologne, Henriette Reker, ameonya juu hatua zitakazochukuliwa zitende haki bila ya kuwaelemea wakimbizi walioingia nchini Ujerumani. Na akachukua hatua ya kufanya mazungumzo ya dharura na maafisa wa polisi kuhusiana na mgogoro huo; ambapo polisi waliahidi kuimarisha ulinzi.