
Hayo yameelezwa leo jijini Dar-es-Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa afya ya uzazi na mtoto kutoka Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii Dk Georgina Msemo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Dkt.Georgina Msemo amesema sababu zinazochangia vifo hivyo ni pamoja na wakina wakinamama wajawazito kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua,kuchelewa kuanza kliniki sambambana kwenda katika vituo vya afya ambavyo havina huduma za kutosha za kumsaidia mama mjamzito wakati wa kujifungua.