Jumanne , 13th Jun , 2023

Mshauri wa mufti wa Tanzania Sheikh bin Zuberi bin Ali katika masuala ya mbambali ya dini na jamii Sheikh Mohamed Iddi Mohamed amewataka viongozi wa dini kukemea waumini wao kutokana na tabia ya watu kuwatusi viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais wa Nchi Dkt Samia Suluhu Hassan 

Amesema si jambo la heri kumtusi kiongozi mkuu wa nchi kutokana na masuala ya kitaifa hata kama kuna utofauti wa itikadi za vyama.

Akizungumza na wandishi wa habari mshauri huyo wa Mufti amesema ili kiongozi uheshimiwe ni lazima kwanza ujenge misingi ya wewe mwenyewe kuheshimu wengine akiwataka watanzania kuacha mihemko kutusi watawala na kuwadhalilisha.

Akihitimisha katika moja ya mapendekezo amesema ni vyema sasa wenye nia ya kupinga mkataba huo wakasema ni maeneo yapi yarekebishwe kwa kuwa tayari Bunge la Tanzania limepitisha azimio la uwepo wa ushirikiano huo wa awali kati ya Tanzania na Serikali ya Dubai.