
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba, alipowasili bungeni kusoma Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Hayo yamebainishwa leo Juni 15, 2023, na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
"Napendekeza kuanzisha programu ya mikopo kwa wanafunzi wanaochaguliwa na serikali kusoma kwenye vyuo vinavyotoa elimu katika fani za kipaumbele ambazo ni sayansi, afya, ufundi na ualimu, hatua hii itaanza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo wa 2023/24," amependekeza Waziri Nchemba
Waziri Mwigulu amesema hatua hiyo inalenga kuongeza idadi ya wataalam na ujuzi unaohitajika katika azima ya mapinduzi ya viwanda.