Jumatano , 3rd Aug , 2022

Jiji la Dar es Salaam limepiga marufuku watu kuwasaidia ombaomba waliokithiri katika maeneo mbalimbali jijini humo huku hatua kali zikitangazwa kuchukuliwa kwa wanaoendelea kuwasaidia.

Ombaomba

Akizungumza na EATV Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto, ambaye amesema kwamba, wameamua kuchukua uamuzi huo katika hatua za kuendelea kulipendezesha jiji la Dar es Salaam, huku akiwataka watu kwenda kutoa misaada kwenye maeneo maalum yaliyotengwa kudhibiti pia biashara haramu ya watu wanaowatumia watoto kuomba hela.