Jumanne , 28th Jun , 2022

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu 25 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uhalifu kwa njia ya mtandao na biashara haramu ya ngono, akiwemo mtu maarufu aitwaye Kigegi anayetuhumiwa kwa wizi wa kimtandao kwa kujifanya mwalimu na mganga

Kanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 28, 2022, Kamanda wa kanda hiyo Jumanne Muliro, amewataja watuhutiwa hao kuwa ni Julius Mwaibula maarufu kama Kigegi na wenzake 22 wanatuhumiwa kwa wizi wa kimtandao wakijifanya walimu na waganga wa kienyeji, pamoja na Marry Sibora (23) na mwenzake wanaotuhumiwa kufanya biashara ya ngono.