Jumanne , 26th Jan , 2016

Wananchi wa Tanzania wametakiwa kulisaidia jeshi la polisi nchini kuwakamata watu wanaofanya mauaji ya watu wenye albinism ili kuondoa sifa hiyo mbaya na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaoikabili nchi kutokana na mauaji hayo.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam Simon mara baada ya kupokea stika zenye ujumbe wa kukomesha mauaji ya watu wenye albinism nchini, stika zilizotolewa na shirika la albinism enterprises kwa kushirikiana na jeshio la polisi.

Aidha Sirro amesema kuwa elimu ya kutosha ikitolewa itasaidia kukokomesha mauaji ya watu wenye albinism kabisa nchini Tanzania na kuondoa sifa hiyo mbaya iliyoko nchini sasa.