Jumanne , 6th Dec , 2022

Wananchi wa mtaa wa Lwenge kata ya Kalangalala mkoani Geita wameanzisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja kwenye shule ya msingi Mseto ili kupunguza changamoto ya wanafunzi zaidi ya 1000 ambao wanatumia  vyumba 12 huku shule hiyo ikiwa na uhitaji wa vyumba 24

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Niyimbona Matiti anasema wana changamoto ya vyumba 12 huku vilivyopo ni chakavu sana na kimoja wapo hukitumika kama ofisi ya walimu.

"Vyumba hivyo 12 ni vichakavu ambapo vitatu tunkati ya hivyo ndivyo wadau vinaweza kuonekana  kama madarasa, shule haina ofisi ya walimu, walimu hutumia chumba cha darasa ambacho pia ni chakavu" alisema Matiti.

Baadhi ya wananchi wa mtaa huo wanasema kwa kujali wanafunzi wanaosoma shule hiyo wakawiwa kuanzisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa. 

"Tumejitolea kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya watoto ni wajibu wetu katika shule hii ya msingi Mseto hii ni kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita", alisema Nzagamba.

"Shule hii ya Mseto iko mjini na ipo katikati ya mji lakini ukiangalia majengo yake yamechakaa kweli yanatia aibu na baadhi ya majengo hapo chini sio salama hata kwa wanafunzi", alisema Butabile. 

"Mahitaji ya kata ya Kalangalala ukiyatekeleza yote kwa asilimia 100 ni zaidi ya asilimia 50 ya bajeti yote ya halmashauri na kumbuka tunazo kata 13 lakini tutaendelea kuwa tunaboresha mahitaji yale yanayokuwa yanawezekana kwa wakati huo", alisema Morandi.

"Kupitia Ofisi ya CCM ni tofali karibia 800 zimechangiwa pale kwahiyo ni wajibu wetu kwa sababu sisi tunaongoza hii jamii na tunaishi kwenye jamii watoto wanaosoma ni watoto wa jamii, tunao wajibu kama chama lakini kama wazazi kushiriki na wananchi kwenye hii kiradi ya maendeleo ", alisema Nyasilu. 

Kaimu mkuu wa wilaya ya Geita ameitaka kamati ya Ujenzi kuwa na matumizi bora ya fedha ili fedha zilizotolewa na wadau kwa ajili ya ujenzi huo ziweze kutumika kwa usahihi.

"Kama tumesema Kokoto ni kiasi fulani tumeagiza kamati tuwe wawazi na wananchi wafahamu, naposema wananchi wafahamu punde baada ya mradi kukamilika lazima tuwaite wananchi wetu tuweze kuwasomea mapato na matumizi, kwa sababu ni haki yao ya kimsingi hivyo naelekeza kwamba mradi unapokamilika tuwe na matumizi bora ya fedha lakini isitoshe tusome mapato na matumizi ili wananchi waweze kufahamu fedha waliyochangia imeweza kufanya kazi gani", alisema