
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mussa Ntimizi wamesema kwamba kilo moja ya sukari inapatikana kwa shilingi elfu tatu hadi elfu tano kwa kilo na kuwaelemea katika bajeti zao za kila siku.
Mmoja wa wafanyabiashara Yona Lukas amesema wao kama wafanyabiashara wanapenda wananchi wapate sukari kwa bei ya kawaida ya 2200 lakini upatikanaji wake umekuwa mgumu ndiyo maana bei zipo juu tena tofauti kutonana na umbali kutoka eneo la upatikanaji hadi kwa wananchi.
Aidha Mbunge wa Jimbo la Igalula Mussa Ntimizi amesema kwamba kero hiyo ataiwasilisha serikalini kwa kuwa serikali iliahidi kwamba wananchi hawata pata kero ya sukari kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani