Jumatano , 29th Oct , 2025

Wananchi wamejitokeza kwa wingi katika Kituo cha Kupigia Kura cha Kariakoo, Jimbo la Kwahani leo Jumatano, kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

 

Foleni ndefu ziliweza kushuhudiwa mapema asubuhi, huku wakazi kutoka maeneo mbalimbali wakionyesha hamasa kubwa na uzalendo katika kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.

Katika uchaguzi huu, wananchi wa Zanzibar wanapiga kura tano muhimu ambazo ni:  
- Rais wa Zanzibar  
- Mbunge  
- Mwakilishi  
- Diwani  
- Diwani wa Viti Maalum

Hatua hii inaonesha uzito wa maamuzi ya wananchi katika kuamua mustakabali wa Taifa kwa miaka ijayo.

Muda mfupi kutoka sasa, Mgombea Urais wa Zanzibar anatarajiwa kupiga kura katika kituo hicho hicho cha Kariakoo, hatua itakayoongeza mvuto wa kisiasa katika eneo hilo.

Tutaendelea kukujuza taarifa zaidi moja kwa moja kutoka vituo mbalimbali vya kupigia kura.