Jumatatu , 22nd Jun , 2015

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii imewaalika wadau muhimu wa habari leo mkoani Dodoma kutoa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari wa mwaka 2015.

Katibu wa jukwaa la wahiriri Tanzania Neville Meena.

Katibu wa kamati hiyo Emmanuel Mdidi amesema kikao hicho cha wadau wa habari kujadili muswada huo ulioibua manung'uniko miongoni mwa wadau wa habari, kinafanyika mkoani Dodoma katika ukumbi wa Pius Msekwa kuanzia majira ya saa tano asubuhi.

Wadau wa habari wamekuwa wakilalamikia vifungu kadhaa vya muswada huo, ambavyo vinaonekana dhahiri vinalenga kukandamiza uhuru wa habari na wa vyombo vya habari nchini Tanzania.

Kutokana na mapungufu hayo Katibu wa jukwaa la wahiriri Tanzania Neville Meena ametaka muswada huo kuahirishwa kabisa kujadiliwa bungeni.