Jumanne , 14th Sep , 2021

Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Majimoto Mpimbwe mkoani Katavi, Emmanuel Shani, ameshangazwa na ujasiri wa baadhi ya wananchi wasio waadilifu kulima bangi ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi, licha ya kuwepo wanyama wakali ikiwemo Simba na Chui lakini wananchi hao hawahofii maisha yao.

Bangi

Kamanda Shani ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Majimoto, kuhusu tabia zao za kulima bangi na kusema pia wapo baadhi ya wananchi hao walipanda bangi katikati ya hifadhi hiyo karibu na Mto Kavuu, mashamba ambayo baadhi yake walifanikiwa kuyateketeza mwezi Julai, 2021.

Tazama video hapa chini