Jumamosi , 19th Mar , 2016

Kamishna wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema jeshi la Polisi litanza kuwakamata watu wanaomiliki silaha nchini mara baada ya kukamilika zoezi la usajili wa silaha kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Kamishna wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Jana Kamishna Sirro amesema kuwa watanzania hawana sababu ya kusbiri mpaka wakamatwe hivyo wajitokeze kuzisajili silaha kabla ya siku ya mwisho ambapo baada ya hapo hatua za kisheria zitafuata.

Kamishna Sirro amewataka wananchi hao wanaomiliki silaha wafike ofisi za maocd na kuwasilisha maelezo ya kutosha juu ya matumizi ya silaha hizo ikiwemo na kama kuna risasi zilizotumika na kuelezea matumizi yake.

Katika hatua nyingine Kamanda Sirro amesema jeshi la polisi mkoa wa Dar es Salaaam limefanikiwa kumkamata Hussein Hariri, ambae ni mtuhumiwa wa usambazaji wa dawa za kulevya kwa mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha katika masuala ya usalama barabarani jeshi hilo pia limefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 577 ikiwa ni tozo kwa madereva wa magari kwa makosa ya barabarani ndani ya wiki mbili ndani ya wiki mbili ndani ya mwezi march.