Ijumaa , 9th Jun , 2023

Jeshi la Polisi mkoani Manyara linawashikilia Juma Athumani (23) na Mariam Mbega (26) kwa tuhuma za kuvunja nyumba  na kuiba Sh milioni 47 za Laurent Elias mfanyabiashara na mkazi wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro.

Imeelezwa kuwa Baada ya uhalifu wa kuiba fedha hizo watuhumiwa  hao walizificha kwa kuziweka kwenye akaunti zao benki ili wasibainike na kukamatwa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara ACP Goerge Katabazi amesema tukio hilo lilitokea Juni 6.2023 katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro

Amesema Jeshi la Polisi limezuia fedha hizo zisitoke huko benki ili taratibu za kisheria zifuatwe na watuhumiwa hao wanashikiliwa na Polisi kwa upelelezi zaidi