
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Rukwa Swagile Msananga (mwenye suti nyeusi) akiwa naTimu ya Uhakiki wa Maeneo ya wazi kutoka Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Rukwa.
Hayo yamesemwa na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Rukwa, Swagile Msananga, akiwa anaongelea zoezi la uhakiki wa maeneo hayo ambapo amesema lengo ni kupata orodha kamili na kutambulika rasmi.
“Kwa maeneo ambayo yatakuwa yamevamiwa, kutakuwa hakuna namna ya kufanya isipokuwa wavamizi wataondolewa ili kupisha maeneo ya wazi kwasababu yanatakiwa yalindwe kwa nguvu zote” alisema Msananga
“Maeneo ambayo yapo salama mpaka sasa hivi tutahakikisha mipaka yake inawekwa bayana na wananchi watatakiwa waiheshimu,” Aliongeza Msananga.
Aidha Kamishna Msananga alisikiliza na kuchukua malalamiko ya mmoja wa wananchi juu ya mgogoro wa ardhi kwa dhumuni la kuyafanyia kazi.