
Kushoto ni muuguzi Scolastica Kanje na Mwalimu Omary Kwesiga, wakiigiza kuchomana chanjo na kulia ni Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu
Aidha Waziri Ummy ameagiza Afisa Muuguzi Msaidizi katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha Scolastica Kanje, aliyekuwa akishirikiana naye katika igizo hilo la uchomaji wa chanjo hiyo kupelekwa kwenye Baraza la Wauguzi na Wakunga kwa hatua zaidi, ambapo Baraza hilo limeagiza muuguzi huyo asimamishwe kazi kwa miezi mitatu.
Hatua hiyo imekuja baada ya video clip kusambaa mitandaoni ikionesha wawili hao kufanya igizo hilo.