Ijumaa , 6th Oct , 2023

Miili ya watoto mapacha  (17) waliopoteza maisha baada ya kupewa dawa za kukuza matiti yazikwa leo kijiji cha Bubale kilichopo kata ya Nkololo halmashauri ya wilaya ya Bariadi. 

majeneza yaliyobeba miili ya watoto

Wakiwa msibani hapo Afisa Ustawi wa Jamii wa halmashuri hiyo Shadrack Nundu, ameisisitiza jamii kufuata ushauri wa wataalamu ili kuepusha vifo visivyotarajiwa huku mkaguzi wa polisi kata ya Nkololo Agnes Henry  akiitaka jamii  kutokutumia njia za mkato kutatua changamoto zikiwemo za  kiafya.

Yohana Saku ni baba mzazi wa watoto hao waliopoteza maisha amesema tayari alikuwa kaanza maandalizi ya kuwapeleka watoto wake shule ili waweze kuendelea na masomo yao badae waje waisaidie familia.

Akiongoza ibada ya mazishi mchungaji wa kanisa la waadventist wasabato ,Chilonge Hezron ameiomba jamii kuachana na imani za kishirikiana na badala yake iwe na hofu ya MUNGU hatua itakayopelekea jamii kuishi kwa kufuata ushauri ulio bora.
Watoto hao walifariki Oktoba 4,2023 na na mara baada ya mazishi yao taratibu za kiserikali zikiendelea.