Jumanne , 16th Aug , 2022

Idadi ya watu waliofariki katika ajali iliyotokea hii leo Agosti 16, 2022, katika eneo la mteremko wa Inyala Pipeline wilayani Mbeya imefikia 19 ambapo kati yao wanaume ni 12 wanawake sita na mtoto mmoja. 

Moja ya gari lililoparamiwa na lori

Aidha  watu 10 wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo ambapo wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Igawilo. Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ulrich Matei amethibitisha usiku huu.

Ajali hiyo imetokea hii leo majira ya saa 2:00 asubuhi, huku chanzo cha ajali kikielezwa kuwa ni kufeli kwa breki ya lori iliyopelekea lori hilo kuparamia magari mengine yaliyokuwa chini ya mlima.