Jumapili , 28th Nov , 2021

Zaidi ya wanafunzi 500 wa Shule ya Msingi Omunga, kakika Wilaya ya Rorya, mkoani Mara, wanalazimika kuchangia vyoo na walimu wao kutokana na shule kukosa vyoo vya kutosha. 

Picha ya mfano wa vyoo

Hayo yameelezwa na Mwalimu  Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Francis Sengo, katika uzinduzi wa Kikundi cha UWAMO kilichoanzishwa kwa ajili ya kuchochea shughuli za maendeleo ya kijijini hapo, ambapo amesema shule hiyo ina matundu sita pekee ya vyoo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Gerald Ng'ong'a, mbali na kukiri uwapo wa changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo shuleni hapo, ameahidi kushirikiana na wananchi kudhibiti adha hiyo huku Kikundi cha UWAMO kimeanza ujenzi wa chumba cha darasa pamoja na nyumba ya walimu, ili kusaidia ukuaji wa elimu kijijini hapo.