na baadhi yao kukaa chini na kuhafifisha suala zima la Ujifunzaji na Ufundishaji.
Baadhi ya wanafunzi na walimu wamesema, uhaba uliopo wa madawati unasababisha baadhi ya wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini na wengine kukaa zaidi ya watatu kwa dawati moja.
Akieleza uhitaji wa Madawati Afisa Elimu Msingi, Vifaa na Takwimu Halmashauri ya Mji Kasulu Michael Yusufu amekili zaidi ya wanafunzi 19 elfu kusoma kwa shida kwa kukosa madawati.
Katika Kukabiliana na Changamoto ya Uhaba wa Madawati, Mbunge wa Jibo la Kasulu Mjini, Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako kupitia Mfuko wa Jimbo amekabidhi madawati 750, kusaidia shule zenye uhaba mkubwa.