Jumapili , 31st Jul , 2016

Wizara ya nishati na madini imeshauriwa kukaa pamoja na wauzaji wa gesi inayotumika katika majiko ya soko la samaki la feri ili wafanyabiashara hao waweze kumudu bei ya gesi na kuondokana na changamoto inayowakabili.

Wakizungumza na East Africa Radio, sokoni hapo wafanyabiashara hao wamesema uwepo wa matumizi ya gesi umeleta changamoto ya kukosa wateja kutokana na wateja kushindwa kumudu bei ya gesi hali inayokwamisha mwenendo wa biashara yao.

Hayo yamebainishwa na mwenye kiti wa wakaanga samaki wa soko Bw. Sirili Peter Nyange ambapo amesema mbadala wa gesi umekuwa ukiwalazimu kutumia gharama kubwa sana katika manunuzi kuliko fedha wanazoingiza kwa biashara hiyo.

Kwa upande wake katibu wa wakaanga samaki wa soko hilo Majuto Ali Majuto amesema hali ya soko kwa kipindi hiki imekuwa mbaya kutokana na kukosa wateja na kuiomba serikali kufanya mazungumzo na wamiliki na wawauzaji gesi.

Isaa Abdallah ni muzaji wa samaki na Pweza ambae ni muathirika wa uwepo wa gesi katika soko hilo amesema kupanda kwa bei ya ukangaji wa samaki kunawadidimiza wafanyabiashara wadogo ambao hutegemea zaidi biashara hiyo katika kupata kipato cha kila siku.