Jumatatu , 3rd Jul , 2023

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko ametoa wito kwa umma kujitokeza kwa wingi kuandamana dhidi ya rais Macky Sall anayewania muhula wa tatu.

Rais Macky Sall sasa anatarajiwa kutoa hotuba baadaye kutangaza iwapo atawania urais mwaka 2024, jambo ambalo wataalamu wengi wa sheria wanasema litakiuka katiba ya Senegal.

Mwezi uliopita, maelfu ya waandamanaji waliingia mitaani katika miji mbalimbali ya Senegal baada ya Sonko kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kuwahonga vijana.

Wafuasi wa Sonko na baadhi ya waangalizi wa kisiasa wanasema kesi hiyo ilikuwa jaribio la kumzuia kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Suala hilo lilisababisha mapigano  yalikuwa mabaya zaidi katika kumbukumbu ya hivi karibuni.

Sonko pia alisema siku ya Jumapili kwamba iwapo rais atatangaza nia ya kuwania muhula wa tatu ni muhimu kwa watu wote wa Senegal kusimama, kukabiliana naye.Katiba hiyo inawazuia marais kuhudumu kwa mihula miwili madarakani lakini wafuasi wa Bw Sall wanasema kuwa hilo linapaswa kurefushwa kwa sababu katiba mpya ilipitishwa mwaka 2016.

Jaribio la kuwania muhula wa tatu wa rais Abdoulaye Wade mwaka 2012 liliitumbukiza nchi hiyo katika ghasia na kusababisha vifo vya watu 12.