Jumatano , 24th Jun , 2015

Wajasiriamali wadogo wametakiwa kutumia fursa za vikoba katika kukuza mitaji ya biashara zao ili kuhimili ushindani wa kibiashara na bidhaa kutoka nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Dkt. Reginald Mengi.

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mauzo ya hisa ya kikundi cha akiba na kukopa cha YETU Microfinace PLC, Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi amesema changamoto inayowakabili wajasiriamali hao ni ukosefu wa mitaji.

Dk. Mengi amesema kuwa mazingira hayatoi fursa kwa mjasiriamali kukuza biashara yake na kujiongezea kipato ama kupanua wigo wa shuguli zake na kwamba wanalazimika kutumia fursa hiyo ya vikoba.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kikundi hicho Altemius Milinge amesema kuanzishwa kwa hisa katika kikundi hicho ni nafasi pekee kwa wajasiriamali hususani wanawake katika kujikwamua kiuchumi.