Mwita Waitara (kushoto) na Gibson Meiseyeki (kulia)
Meiseyeki ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv ambapo amesema anaheshimu hadhi aliyopatiwa na wananchi wa Arumeru kuwa ni miongoni mwa wabunge walifanikiwa kushinda majimbo yao kwa kupata kura nyingi.
Mbunge huyo amesema “nataka nikwambie huyu ndugu nafikiri ana matatizo ya akili, na kama ufahamu mimi ndiye mbunge niliyeshinda kwa tofauti ya kura nyingi kuliko kwa wabunge wote wa Tanzania siwezi kuwaangusha wananchi wangu kwa kutangatanga.”
"Waitara mngemuangalia kama alikuwa amelewa maana akipata bia mbili anakuwa kama amevuta bangi, wakati mwingine muwapime kabla hajongea, sijui ameziokota wapi yeye sijawahi kuzungumza na yeye akiwa CHADEMA au baada ya kutoka CHADEMA, namwambia apambane na hali yake kwa kuangalia matatizo yake". ameongeza Mbunge huyo.
Mapema mwezi huu, Mbunge mteule wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara aliwahi kunukuliwa akisema, "katika zile Arumeru mbili mbunge mmoja atahama muda si mrefu, na hapa Dar es salaam kuna mbunge mmoja atahama, nilisema wabunge watano wamesharudi wawili, tayari Marwa Ryoba, na James Ole Milya wamesharudi, kwa hiyo tutegemee jambo lolote kuanzia sasa kwa wabunge wa mkoa wa Dar es salaam na Arusha."
