Jumatano , 22nd Jun , 2022

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala, ametangaza kuanza kwa oparesheni maalum ya siku kumi kwa ajili ya kuwasaka wahamiaji haramu katika eneo la Loliondo na Ngorongoro mkoani Arusha.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala

Kamishna Jenerali Makakala amebainisha hayo leo Juni 22, 2022, katika Tarafa ya Loliondo, na kusema kuwa zoezi hilo litaenda sawia na zoezi linaloendelea la uwekaji wa alama za mipaka katika pori Tengefu la Loliondo.

"Nchi yetu imebarikiwa kwa kuwa na maeneo mazuri ambayo yanavutia wahamiaji haramu kufika nchini kwa sababu tofauti, hatutakubali hilo litokee wakati wowote ule," amesema Kamishna Makakala.

Dkt. Makakala amesisitiza kufuatwa kwa sheria za nchi  pale wageni wanapotaka kuingia au kutoka nchini, na kwamba Uhamiaji wamejipanga vema kusimamia eneo hilo katika mipaka yote nchini.