barabara ya kuingia soko hilo la soweto jijini mbeya
Wananchi hao wameeleza kusikitishwa kwao kutokana na halmashauri ya jiji la Mbeya, kudaiwa kushindwa kukarabati barabara za eneo la Soweto, na wananchi kulazimika kutotumia mwendo mrefu kufuata huduma za kijamii.
Wafanyabiashara hao wamesema kuwa wateja wao wanashindwa kuingia dukani kutokana na maji hayo kuzunguka maduka lakini pia wanashindwa kushusha bidhaa zao eneo hilo kutokana na kutoa kuwa salama kiafya kwa sababu ya kukwama kwa maji kwa miezi mitatu hivi sasa.
Kwa upande wake Kaimu wa Halmshauri ya Jiji la Mbeya Vicent Msola,amesema tangu kukamilishwa kwa miundombinu iliyofadhiliwa na benki ya dunia barabara nyingi ambazo hazikuhusika na mradi huo zimekua ni tatizo kubwa.



