
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jafo
Ameyasema hayo katika uzinduzi wa Wiki ya Maonesho ya Ufugaji wenye Tija na Utunzaji wa Mazingira sanjari na kuzindua Chama cha Mazingira na Ufugaji Tija Tanzania (CHAMAUTA) katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambapo amesema ufugaji endelevu usioathiri hifadhi ya mazingira utasaidia kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji nchini.
“Tuepuke migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambayo tunashuhudia ikitokea katika baadhi ya mikoa nchini husababisha kutoelewana kwa makundi haya mawili hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani,”amesisitiza Waziri Jafo.