Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi, amesema wafuasi hao waliwafanyia fujo wafuasi wa chama cha mapinduzi ccm wakati wakitoka katika kampeni za mgombea wa urais kupitia chama hicho.
Kamanda ameeleza kuwa kufuatia vurugu hizo jeshi la polisi lililazimika kutumia nguvu kuwatawanyisha watu hao ambapo 62 walishikiliwa na polisi na baadae 48 wakaachiliwa kwa dhamana huku 14 wakipandishwa kizimbani.
Aidha Kamanda Mundi amewataka wanasiasi kutumia kitabu cha maadili ya uchaguzi kwa kutoa elimu kwa wafuasi wa vyama vyote juu ya sheria ya ufanyaji wa kampeni ili kuepuka uvunjifu wa amani kwa kufanya kampeni za kistarabu.
Hata hivyo ameongeza kwa kutoa wito kwa wanasiasa wote pamoja na wafuasi kufuata sheria za kampeni na kuepusha vurugu zisizo na ulazima kutokana na kuwa siasa sio ugomvi.